1 Chronicles 29:22-25

22 aWakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele za Bwana siku ile.

Wakamtawaza Sulemani mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili ya Bwana ili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani.
23 bSulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha Bwana kuwa mfalme mahali pa Daudi baba yake. Akafanikiwa sana na Israeli wote wakamtii. 24 cMaafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Sulemani.

25 d Bwana akamtukuza sana Sulemani mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.

Muhtasari Wa Utawala Wa Daudi

Copyright information for SwhKC